TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO MKUU WA WANAHISA WA AFRICA50 NA JUKWAA LA MIUNDOMBINU AFRIKA.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akizungumza jambo wakati wa alipofanya Mkutano na Wanahabari, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam, ambapo alisema Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Taasisi ya Africa50 pamoja na Jukwaa la Miundombinu Afrika (Infra for Africa Forum), uliobeba kaulimbiu ya “Miaka kumi ya mafanikio kutoka maono hadi utekelezaji - A Decade of Economic Impact: From Ambition to Delivery.” utakaofanyika tarehe 5 na 6 Agosti 2026 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam, ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi na Mwenyekiti wa hafla ya ufunguzi wa mkutano huo.
