Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

WIZARA YA FEDHA YAWAKARIBISHA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LA WIZARA KATIKA MAONESHO YA SABASABA 2026

28 Jun, 2026
WIZARA YA FEDHA YAWAKARIBISHA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LA WIZARA KATIKA MAONESHO YA SABASABA 2026

Mwandishi Mwendesha Ofisi Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bi. Masia Msuya, akiwasainisha kitabu cha wageni wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yenye Kaulimbiu kuu "Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ni Fahari ya Tanzania", yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, jijini Dar es Salaam.

 

Wizara ya Fedha imetoa wito kwa wananchi, wafanyabiashara, na wadau mbalimbali wa uchumi kutembelea Banda la Maonesho la Wizara ya Fedha, ili kupata huduma zinazotolewa na Wizara kupitia Wizara yenyewe na Taasisi zilizochini yake, hatua inayolenga kuimarisha uwazi na uwajibikaji kati ya Wizara na wananchi.

Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanafanyika katika Viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, jijini Dar es Salaam, kuanzia Juni 28 hadi Julai 13, 2026, yakiwa na Kaulimbiu kuu "Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ni Fahari ya Tanzania" ikiwa ni sambamba na kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Maonesho hayo.

Lengo kuu la ushiriki wa Wizara na Taasisi zake katika Maonesho hayo ni kusogeza huduma karibu na jamii na kutoa elimu ya kifedha itakayosaidia kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Serikali, usimamizi wa rasilimali za Taifa na fursa na huduma mbalimbali za masomo na kiuchumi zinazopatikana nchini.

Maafisa kutoka Idara na Vitengo mbalimbali vya Wizara ya Fedha na Taasisi zake, wanaoshiriki maadhimisho hayo ni pamoja na Maafisa kutoka Idara ya Bajeti, Idara ya Pensheni, Idara ya Usimamizi wa Sera za Ununuzi wa Umma, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Idara ya Uchambuzi wa Sera, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi.

Aidha, katika Banda la Wizara ya Fedha, Watumishi kutoka Taasisi mbalimbali za Wizara hiyo, wanapatikana ili kutoa huduma kwa wananchi na wafanyabishara wote, ikiwemo watumishi kutoka Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Mfuko wa uwekezaji wa Utt Amis, Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM), na Soko la Hisa la Dar Es salaam (DSE).

Taasisi nyingine zinazopatikana katika Banda la Wizara ya Fedha ni pamoja na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi  wa Hesabu Tanzania (NBAA), Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA), Mfuko wa Self (Self Microfinance), Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA), Benki ya Maendeleo (TIB), Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA),  Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini (GPSA), Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (TOST) pamoja na Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP).

Wananchi wote wanakaribishwa kutembelea Banda hilo, ambapo wataalamu waliobobea kutoka Idara na Taasisi mbalimbali zilizo chini ya Wizara wapo tayari kutoa huduma na ufafanuzi wa kina kuhusu masuala ya sera za kodi, bajeti kuu ya Serikali, na pamoja na huduma mbalimbali zinazotolewa na Wizara ya Fedha na taasisi zake.

MWISHO.