Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

SERIKALI YASHAURIWA KUANZISHA KLABU ZA MASUALA YA FEDHA SHULENI

14 Aug, 2024
SERIKALI YASHAURIWA KUANZISHA KLABU ZA MASUALA YA FEDHA SHULENI
Serikali imeshauriwa kuwasimamia Wakuu wa Shule kuongeza kasi ya kuanzisha Klabu za mambo mbalimbali yakiwemo masuala ya fedha katika shule zilizopo nchini ili zitumike kutoa elimu hiyo pamoja na mambo ya kijamii.
 
Ushauri huo umetolewa na Mlezi wa Klabu katika Shule ya Sekondari ya Kutwa Liwale, Mwalimu Mustafa Ahmadi Likambako, alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha ambayo ipo mkoani Lindi kutoa elimu ya masuala ya fedha kwa makundi mbalimbali ya wananchi wakiwepo wanafunzi, wafanyabiashara, wakufunzi na wajasiriamali.
 
“Katika shule yetu tuna Klabu tatu ya mazingira, masuala ya rushwa na femina, kwakuwa mimi ndio mlezi wa clubs hizi nimeona zinavyowasaidia wanafunzi kuwa na uelewa mpana wa masuala ya kijamii  wanayojifunza muda wa ziada”, alisema Bw. Likambako.
 
Aliongeza kuwa upo uhitaji wa Wizara ya Fedha kuona umuhimu wa kuanzisha Klabu ya masuala ya fedha katika shule mbalimbali ili wanafunzi wafundishwe matumizi ya fedha tangu wakiwa wadogo ili wakiwa wakubwa wawe na uelewa wa masuala ya fedha.
 
“Shuleni kwetu tuna matamasha mbalimbali huwa tunatumia jukwaa hilo kuwashindanisha wanafunzi wa Klabu mbalimbali na kutoa zawadi hii inasaidia kumfanya mwanafunzi awe makini darasani lakini kuwa na juhudi binafsi yakusoma na kushika wanachofundishwa”, alisema Bw. Likambako.
 
 Aliongeza kuwa zikianzishwa Klabu za masuala ya fedha katika shule itasaidia kupata mabalozi ambao ni wanafunzi na wakirudi nyumbani likizo wanakua walimu wazuri kwa wazazi wao na jamii inayowazunguka
 
Naye Afisa Mchambuzi Hesabu Mwandamizi, kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana Bi. Mariam Omari Mtunguja, alisema kuwa wametoa elimu ya masuala ya fedha kwa makundi mbalimbali wakiwepo wanafunzi, wakufunzi, vikundi vya wajasiriamali na wafanyabiashara.
 
“Tumeona kiu ya wanafunzi kuuliza maswali mengi wakitaka kujua mitaji inatakiwa kuanzia shilingi ngapi, lakini waliuliza kama wanafunzi wanaruhusiwa kuwa wawekezaji nimeona kuna umuhimu wa elimu hii kuanza kutolewa mapema katika shule mbalimbali”, alisema Bi. Mtunguja.
 
Kwa upande wake, mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Liwale Day Bi. Zuleikha Hamidu, aliahidi kuanza kuweka akiba kwenye fedha za matumizi anazopewa na wazazi wake ili ziweze kumsaidia kwa baadae.
 
Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) na Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC), ipo mkoani Lindi kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha kwa wananchi wa makundi mbalimbali ikiwemo wafanyabiashara, wanavikundi mbalimbali, wajasiriamali, wakufunzi na wanafunzi.