Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

MHE. DKT. NCHEMBA ASHIRIKI MKUTANO WA 24 WA MAWAZIRI WA FEDHA AFRIKA WANACHAMA WA BENKI YA DUNIA NA IMF

05 Aug, 2024
MHE. DKT. NCHEMBA ASHIRIKI MKUTANO WA 24 WA MAWAZIRI WA FEDHA AFRIKA WANACHAMA WA BENKI YA DUNIA NA IMF
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akifuatilia hotuba ya Makamu wa Rais wa Nigeria, Mhe Kashim Shettima (Hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa 24 wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za nchi za Afrika ambazo ni Wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) (Africa Caucus Meetings) unaofanyika katika Hoteli ya Transcorp Hilton, mjini Abuja Nchini Nigeria, ambao unajadili namna ya kuboresha biashara katika nchi za Afrika kwa kuweka mazingira mazuri ya kusisimua biashara kwa kujenga miundombinu itakayowezesha kukuza biashara miongoni mwa nchi za Afrika na wataweka msimamo wa pamoja na kupeleka agenda ya namna  Taasisi za Fedha za Kimataifa ikiwemo Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, zinatakiwa kuziwezesha nchi hizo kifedha na kiutaalam ili zifikie malengo husika.
 
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 24 wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za nchi za Afrika ambazo ni Wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) (Africa Caucus Meetings) unaofanyika katika Hoteli ya Transcorp Hilton, mjini Abuja Nchini Nigeria. Mkutano huo umefunguliwa rasmi tarehe 2 Agosti, 2024 na Makamu wa Rais wa Nigeria, Mhe Kashim Shettima.
 
Mkutano huo unajadili namna ya kuboresha biashara katika nchi za Afrika kwa kuweka mazingira mazuri ya kusisimua biashara kwa kujenga miundombinu itakayowezesha kukuza biashara miongoni mwa nchi za Afrika na wataweka msimamo wa pamoja na kupeleka agenda ya namna  Taasisi za Fedha za Kimataifa ikiwemo Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, zinatakiwa kuziwezesha nchi hizo kifedha na kiutaalam ili zifikie malengo husika.