Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

MHE BALOZI OMAR AIPONGEZA NMB KWA MCHANGO WAKE KATIKA KUKUZA UCHUMI WA NCHI.

20 Jul, 2026
MHE BALOZI OMAR AIPONGEZA NMB KWA MCHANGO WAKE KATIKA KUKUZA UCHUMI WA NCHI.

Waziri wa Fedha, Mhe. Khamis Mussa Omar (Mb), akiagana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hya NMB, Bi. Ruth Zaipuna baada ya Mkutano kati yao kuhusu ushirikiano, uliofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.

 

Waziri wa Fedha, Mhe. Khamis Mussa Omar (Mb), ameipongeza Benki ya NMB kwa mchango wake katika kuisaidia Serikali kupitia ukusanyaji wa mapato pamoja na utoaji wa huduma mbalimbali za kifedha zinazowanufaisha wananchi.

Mhe. Balozi Omar alitoa pongezi hizo alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Benki ya NMB ulioongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Bi. Ruth Zaipuna, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.

Alisema NMB imeendelea kuwa mshirika muhimu wa Serikali kwa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, huku akieleza kuwa Serikali inatarajia mafanikio makubwa zaidi katika mwaka 2026 kupitia ushirikiano huo.

“Kwa ujumla mmefanya kazi nzuri, ikiwemo upande wa gawio. Tunaamini Serikali itaendelea kushirikiana na NMB katika maeneo mbalimbali, yakiwemo ya ukusanyaji wa kodi na utoaji wa huduma nyingine za kifedha,” alisema Mhe. Balozi Omar.

Aliongeza kuwa Serikali inafurahishwa na mafanikio yaliyofikiwa na benki hiyo na itaendelea kuiunga mkono ili iweze kutekeleza wajibu wake wa kuchangia maendeleo ya uchumi wa nchi.

Mhe. Balozi Omar pia aliipongeza NMB kwa kuanza vyema utekelezaji wa Mpango Mkakati wake mpya wa miaka mitano, akisema ana matumaini benki hiyo itaendelea kukua, kupanua huduma zake na kuimarisha nafasi yake katika uchumi wa Taifa.

Alisema NMB ni miongoni mwa taasisi za kifedha zinazoshirikiana kwa karibu na Serikali, jambo linalofungua fursa zaidi za ushirikiano katika kuhudumia taasisi za umma na miradi ya maendeleo.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna, alisema benki hiyo imezindua huduma mpya ya mikopo ya kidijitali inayowawezesha wateja kukopa hadi shilingi milioni mbili bila kufika katika tawi.

Alieleza kuwa mfumo huo hutathmini historia ya miamala ya mteja na kuamua kiwango cha mkopo anachostahili kwa njia ya kidijitali, hivyo kurahisisha upatikanaji wa mikopo kwa wananchi.

Bi. Zaipuna Alibainisha kuwa huduma hiyo inalenga kuwawezesha zaidi wafanyabiashara wadogo na wa kati pamoja na wanawake kwa kuwapa fursa rahisi ya kupata mitaji ya kuendesha shughuli zao za kiuchumi.

Aidha, alisema benki inaendelea kutoa elimu ya fedha kwa wananchi ili kuwasaidia kutumia mikopo kwa tija na kurejesha kwa wakati, hatua inayochangia kuimarisha nidhamu ya kifedha na kupunguza changamoto zinazotokana na ukosefu wa uelewa wa masuala ya fedha.

Bi. Zaipuna alisema kuwa mbali na huduma za kifedha, NMB imeendelea kutekeleza miradi ya uwajibikaji kwa jamii (CSR), ikiwemo ujenzi na ukarabati wa shule ya watoto wenye mahitaji maalumu katika eneo la Bahi, mkoani Dodoma, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo.

Alisisitiza kuwa NMB itaendelea kuwekeza katika teknolojia, kuboresha huduma za kidijitali na kushirikiana na Serikali pamoja na wadau mbalimbali ili kuongeza upatikanaji wa huduma za benki kwa wananchi kwa urahisi, usalama na ufanisi.

Mwisho