Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

BENKI YA DUNIA YAIMWAGIA SIFA TANZANIA UJENZI WA SGR

05 Aug, 2024
BENKI YA DUNIA YAIMWAGIA SIFA TANZANIA UJENZI WA SGR
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (Katikati), Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (kushoto) na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Viktoria Kwakwa, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao chao, kilichofanyika kando ya Mkutano wa 24 wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za nchi za Afrika ambazo ni Wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) (Africa Caucus Meetings) unaofanyika katika Hoteli ya Transcorp Hilton, mjini Abuja Nchini Nigeria.
 
 
BENKI ya Dunia imeipongeza Tanzania kwa hatua kubwa iliyopiga katika kutekeleza mradi wa kimkakati wa Reli ya Kisasa-SGR kwa kuwa ni miongoni mwa miradi itakayochochea ukuaji wa uchumi wa nchi pamoja na kuboresha huduma ya usafiri na usafirishaji kwa wananchi.
 
Pongezi hizo zimetolewa mjini Abuja nchini Nigeria na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa, alipokutana na ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Kando ya Mikutano wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za Nchi za Afrika, ambazo ni wanachama wa Benki ya Dunia na Shiruka la Fedha la Kimataifa-IMF.
 
Dkt. Victoria Kwakwa, amesema kuwa si rahisi kwa nchi nyingi za Afrika kujenga mradi mkubwa wa reli kama ilivyofanya Tanzania kwa kuwa ina gharama kubwa lakini kukamilika kwake kutachochea biashara katika eneo la Maziwa Makuu huku akimmwagia sifa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuzindua rasmi safari za treni hiyo kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma.
 
Kwa Upande wao, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Natu El-maamry Mwamba, walipokea pongezi hizo kwa niaba ya Serikali na kueleza kuwa lengo la mradi huo ni kuunganisha baadhi ya nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki ili kufungua milango ya biashara.
 
Dkt. Nchemba alitumia mazungumzo hayo kuzitaka Taasisi za Fedha za Kimataifa ikiwemo Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, kuangalia uwezekano wa kuweka riba nafuu kwenye mikopo inayotolewa kupitia madirisha ya ujenzi wa miundombinu ili nchi za Afrika ziweze kuboresha miundombinu ya usafiri na usafirishaji hatua itakayochangia kukamilisha miradi husika kwa wakati.
 
Benki ya Dunia ni mdau mkubwa wa maendeleo ya Tanzania ambapo imewekeza kiasi kikubwa cha fedha katika miradi mbalimbali ya kimkakati ya maendeleo pamoja na kuchangia Bajeti Kuu ya Serikali.
 
MWISHO