Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

BALOZI WA ZIMBABWE ATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA FEDHA SABASABA.

30 Jun, 2026
BALOZI WA ZIMBABWE ATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA FEDHA SABASABA.

Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania Mhe. Helen Bawange Dingani, akiagana na Afisa Habari Mwandamizi Wizara ya Fedha, Bw. Ramadhani Kissimba, baada ya kutembelea Idara, Vitengo na Taasisi za Wizara ya Fedha, katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, jijini Dar es Salaam, yakiwa na Kaulimbiu kuu "Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ni Fahari ya Tanzania".

 

Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Mhe. Helen Bawange Dingani, ametembelea Banda la Maonesho la Wizara ya Fedha, katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, jijini Dar es Salaam, yakiwa na Kaulimbiu kuu "Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ni Fahari ya Tanzania".

Mhe. Balozi alitembelea Idara, Vitengo na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha, ambapo alipata maelezo ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara pamoja na Taasisi zake pamoja na umuhimu wa ushiriki wa Wizara katika maonesho haya ikiwa na lengo la kusogeza huduma kwa jamii.

Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, jijini Dar es Salaam, kuanzia Juni 28 hadi Julai 13, ni maonesho ya 50 toka kuanza kwake ambapo yanaambatana na kuadhimisha miaka 50 ya maonesho hayo.

MWISHO.