WIZARA YA FEDHA YAENDELEA NA MAPITIO YA SHERIA YA UNUNUZI WA UMMA SURA YA 410 KUENDANA NA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050.
Wizara ya Fedha inaendelea na mchakato wa kupitia upya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura ya 410, kwa lengo la kuioanisha na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, kupitia kikao kazi kilichowakutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta ya umma na binafsi.
Mchakato huo umeanza kwa kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa St. Gasper, Jijini Dodoma, ambapo wadau walipata fursa ya kutoa maoni na mapendekezo yatakayosaidia kuboresha Sheria hiyo.
