TANZANIA YAIHAKIKISHIA FITCH UCHUMI WENYE MWELEKEO CHANYA
Serikali imesema uchumi wa Tanzania unaendelea kuimarika na kwamba uwekezaji katika sekta mbalimbali, hususani madini, gesi, nishati, kilimo na miundombinu, unatarajiwa kutoa msukumo mkubwa kwa ukuaji wa uchumi.
Hayo yalielezwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), wakati akifungua mkutano na wataalamu wa Kampuni ya Kimataifa ya Tathmini ya Madeni ya (Fitch Ratings), uliofanyika kwa njia ya mtandao, ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kufanya mapitio ya hali ya uchumi wa Tanzania.
