TANZANIA NA MAREKANI ZAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO KATIKA NISHATI, AFYA NA UWEKEZAJI.
Tanzania na Marekani zimeendelea kusisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa kimkakati katika sekta mbalimbali zikiwemo madini adimu, nishati, afya, uwekezaji na maendeleo ya kiuchumi, pamoja na dhamira ya kuendeleza mazungumzo na ushirikiano wa kitaalamu kwa manufaa ya nchi hizo mbili.
Hayo yameafikiwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mhe. Andrew Lentz, walipokutana na kufanya mazungumzo ya katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, ambapo pia walieleza umuhimu wa kuendelea kutumia majadiliano ya kitaalamu na ushirikiano wa Serikali kwa Serikali katika kushughulikia maeneo yenye umuhimu wa kimkakati, ikiwemo maendeleo ya sekta ya Nishati ya Gesi Asilia (Liquefied Natural Gas (LNG).
