SERIKALI, BENKI YA DUNIA ZAKAMILISHA MAANDALIZI YA PROGRAMU YA KAZI MPA.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Kida, ameongoza Ujumbe wa Serikali ya Tanzania kwa niaba ya Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, katika kikao na Ujumbe wa Benki ya Dunia kilicholenga kuhitimisha maandalizi ya kitaalamu ya Programu ya Uendelezaji wa Ushoroba wa Kati wa Maendeleo ya Kiuchumi Utakaoongeza Ajira kwa Vijana (CATALYZING JOBS AND RESILIENT GROWTH IN THE CENTRAL CORRIDOR MULTIPHASE PROGRAMMATIC APPROACH (KAZI MPA). Kikao hicho kilifanyika kwa lengo la kuwasilisha na kujadili matokeo ya maandalizi yaliyofanywa kwa pamoja kati ya Serikali na Benki ya Dunia, pamoja na kukubaliana hatua zinazofuata kuelekea kukamilisha maandalizi ya Programu hiyo, kilichofanyika, Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.