Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, ameyashauri Mabaraza ya Rufani za kodi na Baraza la Rufaa nchini kuharakisha utoaji wa hukumu za kesi zinazohusu kodi ili kuiwezesha serikali kukusanya kodi yake kwaajili ya maendeleo ya nchi...

Mens Footwear Online paypal

 

Dkt. Kijaji ametoa ushauri huo Jijini Dar es salaam wakati akizundua kitabu chenye ripoti ya kesi mbalimbali zinazohusu kodi kilichotolewa na Mabaraza hayo ambapo takwimu zinaonesha kuwa kuna kesi zinazofikia thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 4 zinanazoendelea kusikilizwa.

Amesema kuwa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2001 hadi Agosti mwaka huu, mashauri yanayohusu mizozo ya kodi yamefikia 1,354 ambapo mizozo 914 imekwisha amuliwa na kubakia kesi 440

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Sera na Mipango Bi. Mary Maganga akizungumza kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, amesema kuwa kuchelewa kwa maamuzi ya kesi za kodi kunaleta usumbufu kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato na kwa walipakodi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Uhariri wa Toleo hilo Dkt. Ongwamuhana Kibuta, amesema kuwa toleo hilo jipya la Tax Law Report ni la tatu kutolewa na lina jumla ya kesi 103 za mwaka 2009/2010 ambapo lengo

lake ni kuwawezesha wadau kufuatilia maamuzi mbalimbali ya kesi hizo wakiwemo wanataaluma na wanafunzi wa sheria kama rejea yao.

Imetolewa na:

Benny Mwaipaja

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Wizara ya Fedha na Mipango

01 Septemba, 2016