Naibu katibu mkuu Wizara ya Fedha na Mipango,
Mwenyekiti Bodi ya Uhariri,
Mwenyekiti Baraza la Rufani za Kodi,
Mwenyekiti Mteule wa Baraza la Rufani za Kodi,
Mhariri Mkuu- Bodi ya Uhariri, ...

Crazy Light Boost 2017 Low


Kamishna Mkuu - Mamlaka ya Mapato Tanzania,
Wadau wa Bodi na Baraza la Rufani za Kodi,
Vyombo vya Habari,
Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana.
Habari za Asubuhi.
Awali ya yote, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehma kwa kutujalia afya njema na kutuwezesha kujumuika pamoja katika tukio hili la leo. Pili, napenda kuwashukuru
2
Wenyeviti na Uongozi wa Mabaraza ya Rufaa za Kodi kwa kunipa heshima ya kuwa Mgeni Rasmi katika hafla hii ya leo na ya kihistoria kwa Taifa letu. Kipekee, nawashukuru na kuwapongeza wote walioshiriki kwa hali na mali kufanikisha maandalizi ya tukio hili. Aidha, napenda kutambua uwepo wa wakilishi wa Taasisi za Fedha za Kimataifa, Kampuni za Uhasibu, Mawakili Wanaosimamia Migogoro ya Kodi, Taasisi za Fedha na Taasisi za Elimu kwa kujumuika nasi katika hafla hii. Kwa pamoja, nawashukuru kwa ushiriki wenu na karibuni sana katika hafla hii fupi.
Ndugu Wageni Waalikwa, Baraza la Rufani za Kodi na Baraza la Rufaa,kwa pamoja vimekuwa vikifanya kazi nzuri katika kushughulikia mizozo ya kodi inayoletwa kama rufaa katika mabaraza hayo. Kati ya mwaka 2001 na Agosti,2016; Rufaa za Kodi 1,354 zimewasilishwa mbele ya Baraza la Rufani za Kodi zikilalamikia madai mbali mbali yahusuyo Kodi ya Mapato, Kodi ya Ongezeko la Thamani, Ushuru wa Forodha, n.k. Rufaa hizo zinajumuisha kodi ya shilingi trilioni 4, lakini pia kuna kesi ambazo kodi yake iko kwenye sarafu ya Dola za Kimarekani zipatazo milioni 443. Kati ya rufaa 1,354; rufaa 914
3
zimefanyiwa maamuzi. Hii ina maana kuwa rufaa 440 bado ziko katika hatua mbali mbali za usikilizwaji. Idadi hii ya kesi ambazo hazijasikilizwa ni kubwa, ukizingatia kuwa wingi wa kesi za kodi zinazowasilishwa kwenye Baraza la Rufani zinazidi kuongezeka mwaka hadi mwaka. Pia, kiwango cha kodi inayolalamikiwa na ambayo haiwezi kukusanywa bila maamuzi kukamilika nacho kimekuwa kikipanda mwaka hadi mwaka. Hali hii inaweza kuathiri utekelezaji wa shughuli za maendeleo.
Ndugu Wageni Waalikwa, miaka ya 2013, 2014 na 2015 ilikuwa na kiwango kikubwa cha kodi iliyobishaniwa inayofikia kiasi cha shilingi milioni 894. Hadi kufikia Agosti 2016, kiwango cha kodi kinachobishaniwa kwa mwaka huu peke yake ni trilioni 2.4. Mwelekeo huu unaonesha kuwa kiwango cha kodi kinacholalamikiwa kitaendelea kupanda mwaka hadi mwaka. Napenda kutoa rai kwa Mabaraza ya Rufaa za Kodi, Mamlaka ya Mapato na wadau wote wa kodi kujipanga vizuri ili kuhakikisha kuwa kila moja anatimiza wajibu wake kwa kuzingatia misingi, sheria na kanuni za kodi. Aidha, wakati umefika sasa kwa watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kutumia vizuri weledi wao, hususan katika eneo la ukadiriaji na
4
utozaji kodi ili kuondoa migogoro isiyoyalazima. Pia, wadau wa kodi kama vile washauri wa walipa kodi wafanye kazi yao kwa weledi wa hali ya juu ili kuondoa ubishani na malalamiko yasiyo na tija kwa pande zote. Nayaagiza Mabaraza ya Rufaa za Kodi kumaliza migogoro hii kwa haraka bila kuathiri ubora wa maamuzi yanayotolewa. Serikali kwa upande wetu tutaendelea kuhakikisha kuwa taasisi za kodi ikiwemo Mamlaka ya Mapato na Mabaraza ya Rufaa za Kodi zinaendelea kuimarishwa na kutengewa bajeti ya kutosha ili zifanye kazi zake kwa ufanisi.
Ndugu Wageni Waalikwa, lengo la kuandaa na kuzindua Tax Law Report ni kuwawezesha wadau wa kodi kujua tumetoka wapi, tupo wapi na tunaelekea wapi, hususan katika eneo la utungaji na utekelezaji wa sera, sheria na kanuni za kodi. Nia ni kuelimishana na kuweka mazingira rafiki ili kila mlipa kodi aweze kulipa kodi stahiki, kwa hiari na kwa wakati. Aidha, Mamlaka ya Mapato Tanzania inapaswa kuboresha huduma kwa wateja, elimu ya kodi kwa umma na kufanya kazi kwa weledi na uadilifu. Kwa kufanya hivyo, tutakuwa tumeweka mazingira rafiki kwa mlipa kodi na hivyo kuiwezesha serikali kukusanya mapato ya kutosha kwa maendeleo ya Taifa
5
letu. Ikumbukwe kuwa, bila kodi hakuna maendeleo; hivyo kila mtu atimize wajibu wake.
Ndugu Wageni Waalikwa,Mabibi na Mabwana, changamoto iliyokuwepo ya ucheleweshaji wa tarehe za rufaa za kodi zinazoenda Mahakama ya Rufaa imeshughulikiwa kwa kiasi kikubwa. Tangu Februari 2016, mmeshuhudia rufaa za kodi zilizokuwa zimelimbikizana Mahakama ya Rufaa zikisikilizwa na kufanyiwa maamuzi. Tutajitahidi kuhakikisha huu unakuwa ni utaratibu wa kudumu katika Mahakama ya Rufaa ili kuweka mazingira rafiki ya kukusanya na kulipa kodi.
Mwisho, niwashukuru tena Bodi nzima ya uhariri ya Tax Law Reports, Mamlaka ya Mapato na wadau wote wanaohusika na mradi huu kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya. Aidha, ni vema tukahakikisha kuwa taarifa hii inaandaliwa kwa lugha zote mbili, hususan Kiswahili kwa sababu walipa kodi wetu wengi wanatumia lugha ya Kiswahili. Niwatakie kila la kheri na mafanikio zaidi katika machapisho yajayo ya Tax Law Reports.
6
Kwa maneno haya mafupi, sasa naomba nisogee kwenye meza ya uzinduzi ili nikamilishe zoezi la kuzindua chapisho hili.