Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amemwapisha Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, Ikulu, Jijini Dar es salaam, baada ya kumteua kushika wadhifa huo jana...

Nike Fingertrap Air Max


Baada ya kuapishwa, Katibu Mkuu huyo amekula kiapo kingine cha maadili mbele ya Kamishna wa Maadili, Jaji (Mst.) Salome Kaganda, ambaye amemtaka kutekeleza majukumu yake kwa uadilifu mkubwa ili kuisaidia nchi kufikia malengo yake ya kuwatumia wananchi katika sekta ya fedha na uchumi
Bw. Doto James anachukua nafasi ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Servacius Likwelile, ambaye Mhe. Rais Dkt. Magufuli, amesema atampangia kazi nyingine.
Doto James, ambaye kitaaluma ni mchumi, alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango akishughulikia sera, atawaongoza manaibu makatibu wakuu wengine watatu walioko katika Wizara ya Fedha na mipango.
Tukio hilo limehudhuriwa pia na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi, Katibu Mkuu Ikulu, Bw. Peter Ilomo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Doroth Mwanyika, na wakuu wa Mamlaka na Taasisi mbalimbali.
Imetolewa na:
Benny Mwaipaja
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango
01 Septemba, 2016