Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi ameishauri Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake kujenga jengo la kudumu katika Viwanja vya maonesho ya Kitaifa ya Wakulima (Nanenane) mkoani Lindi katika viwanja vya Ngongo ili kupunguza gharama za kukodi maturubai wakati wa maonesho.

Nike Zoom Kobe Shoes

 

Alisema pamoja na kupunguza gharama, baada ya maonesho, jengo hilo linaweza kutumiwa katika shughuli nyingine na Halmashauri ya Wilaya hivyo kuiongezea Wizara kipato.

Mhe. Zambi alitoa ushauri huo alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake katika viwanja vya Ngongo Lindi ambapo aliweza kuona shughuli mbalimbali zilizokuwa zikifanyika katika mabanda ya yanayotumiwa na Taasisi zilizoko chini ya Wizara hiyo.

Vilevile alizishauri Taasisi kujitangaza ili wananchi wengi waweze kufahamu huduma zinazotolewa na Taasisi hizo kwani huduma zao ni muhimu kwa Wananchi hususani wakulima.

"Wananchi wengi wanaoishi mikoani hususani Lindi, hawana uelewa wa kutosha kuhusu huduma

zinazotolewa na Taasisi zilizo chini ya Wizara hasa huduma ya Bima na Mifuko ya uwekezaji"Alisema Zambi.

Alisema kuwa maonesho haya yanawawezesha Wananchi kuelewa pia namna ya utekelezaji wa bajeti na vipaumbele vyake kamavile kujenga miundombinu ya Barabara, Maji, Elimu na Afya.

Mhe. Zambi ameziomba Taasisi zinazoshughulika na utoaji mikopo kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini hasa wakulima ili waweze kujiendeleza kiuchumi.

Pia aliipongeza Serikali kwa kuandaa Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano ambao anaamini utakua chachu ya mapinduzi ya kiuchumi kwani mpango huo umelenga zaidi katika kukuza viwanda ambayo vitaongeza ajira kwa vijana.

Pia alitoa rai kwa Taasisi ambazo hazijashikiri maonesho hayo mwaka huu kujipanga kwa ajili ya mwakani kwani maonesho hayo ni muhimu kwao, Wananchi na Taifa kwa ujumla.

Imetolewa na:

Benny Mwaipaja

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Wizara ya Fedha na Mipango

5.8.2016