• Tanzania kutekeleza mpango mkakati wa AU

  Naibu Katibu Mkuu, Bw. Adolf Ndunguru, akiwa katika warsha ya Kamisheni ya AU

 • Mkurugenzi Mtendaji wa WB, Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, akiangalia shughuli za wajasiriamali

  Mkurugenzi Mtendaji wa WB, Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, akiangalia shughuli za wajasiriamali

 • Mkurugenzi Mtendaji wa WB, Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, akiangalia ujenzi wa Reli ya Kisasa

  Mkurugenzi Mtendaji wa WB, Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, akiangalia ujenzi wa Reli ya Kisasa

 • Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Jafo na wadau wengine wakizindua Mpango Kazi wa Uendelezaji Miji

  Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Jafo na wadau wengine wakizindua Mpango Kazi wa Uendelezaji Miji

 • Mkurugenzi Mtendaji wa WB Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagamba katika Mkutano na Waziri Dkt. Mpango

  Mkurugenzi Mtendaji wa WB Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagamba katika Mkutano na Waziri Dkt. Mpango

 • Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB, Bw. Charles Singili akieleza jambo kwa Dkt. Khatibu Kazungu

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB, Bw. Charles Singili akieleza jambo kwa Dkt. Khatibu Kazungu

 • Katibu Mkuu Bw. Doto James Mwakilishi Mkazi wa Benki AfDB, Bw. Alex Mubiru wakibadilishana hati za mikataba

  Katibu Mkuu Bw. Doto James Mwakilishi Mkazi wa Benki AfDB, Bw. Alex Mubiru wakibadilishana hati za mikataba.

 • Katibu Mkuu Bw. Doto James na Mwakilishi Mkazi wa AfDB, Bw. Alex Mubiru wakitia saini mikataba

  Katibu Mkuu Bw. Doto James na Mwakilishi Mkazi wa AfDB, Bw. Alex Mubiru wakitia saini mikataba.

 • Waziri Dkt. Mpango akiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla ya kuwaaga watumishi wanaokwenda masomoni Uingereza.

  Waziri Dkt. Mpango akiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla ya kuwaaga watumishi wanaokwenda masomoni Uingereza.

 • Naibu Katibu Mkuu Dkt. Khatibu Kazungu akipeana mkono na Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE

  Naibu Katibu Mkuu Dkt. Khatibu Kazungu akipeana mkono na Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE

 • Naibu Katibu Mkuu Dkt. Khatibu Kazungu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa kutoka CMSA na Wizara hiyo.

  Naibu Katibu Mkuu Dkt. Khatibu Kazungu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa kutoka CMSA na Wizara hiyo.

 • Dkt. Kazungu akipeana mkono na Mkuu wa Chuo cha EASTC, Dkt. Mkumbo

  Dkt. Kazungu akipeana mkono na Mkuu wa Chuo cha EASTC, Dkt. Mkumbo

 • Makabidhiano ya ofisi kati ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la NIC. Bw. Sam Kamanga Dkt. Elirehema Doniye

  Makabidhiano ya ofisi kati ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika  la NIC. Bw. Sam Kamanga Dkt. Elirehema Doniye

 • Waziri Dkt. Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Benki AfDB

  Waziri Dkt. Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Benki AfDB

 • Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Doto James akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya wakurugenzi wa sera

  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Doto James akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya wakurugenzi wa sera

 • Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu KATIKA ziara ya kikazi GPSA, Jijini Dar es Salaam.

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu KATIKA ziara ya kikazi GPSA, Jijini Dar es Salaam.

 • Dkt. Khatibu Kazungu akimsikiliza kwa makini Kamishna Mkuu wa TRA, kuhusu changamoto za Mamlaka hiyo

  Dkt. Khatibu Kazungu akimsikiliza kwa makini Kamishna Mkuu wa TRA, kuhusu changamoto za Mamlaka hiyo.

 • Mwaandishi Vitabu Nchini Bw. Richard Mabala akipata maelezo ya Mfumo wa GePG, katika Maonesho ya Nanenane

  Mwaandishi Vitabu Nchini Bw. Richard Mabala akipata maelezo ya Mfumo wa  GePG, katika Maonesho ya Nanenane.

 • Washiriki wa Maonesho ya 43 Sabasaba, wakifurahia tuzo

  Washiriki wa Maonesho ya 43 Sabasaba, wakifurahia tuzo

 • Makamu wa Pili wa Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi akikabidhi tuzo

  Makamu wa Pili wa Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi akikabidhi tuzo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amemwapisha Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, Ikulu, Jijini Dar es salaam, baada ya kumteua kushika wadhifa huo jana...


Baada ya kuapishwa, Katibu Mkuu huyo amekula kiapo kingine cha maadili mbele ya Kamishna wa Maadili, Jaji (Mst.) Salome Kaganda, ambaye amemtaka kutekeleza majukumu yake kwa uadilifu mkubwa ili kuisaidia nchi kufikia malengo yake ya kuwatumia wananchi katika sekta ya fedha na uchumi
Bw. Doto James anachukua nafasi ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Servacius Likwelile, ambaye Mhe. Rais Dkt. Magufuli, amesema atampangia kazi nyingine.
Doto James, ambaye kitaaluma ni mchumi, alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango akishughulikia sera, atawaongoza manaibu makatibu wakuu wengine watatu walioko katika Wizara ya Fedha na mipango.
Tukio hilo limehudhuriwa pia na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi, Katibu Mkuu Ikulu, Bw. Peter Ilomo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Doroth Mwanyika, na wakuu wa Mamlaka na Taasisi mbalimbali.
Imetolewa na:
Benny Mwaipaja
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango
01 Septemba, 2016